Bayern Munich wanaripotiwa kupiga hatua katika harakati zao za kutaka kumsajili Nordi Mukiele kutoka Paris Saint-Germain.
Kulingana na Sky Germany, Mukiele amejitolea kwa Bayern, ambao wana matumaini kwamba dili la mkopo linaweza kukamilishwa.
Gazeti la Bild linaripoti kwamba mkurugenzi wa michezo Christoph Freund hakusafiri hadi kwenye kambi ya mazoezi ya Bayern nchini Ureno alipokuwa akifanya kazi ili kumaliza mkataba huo, huku harakati zikitarajiwa siku chache zijazo.
Freund alizungumza kuhusu uvumi huo katika mahojiano ya hivi majuzi na Bild, akiambia jarida la udaku la Ujerumani:
“Sitaki kutaja majina, lakini kwa ujumla, Nordi ni aina ya mchezaji anayeweza kucheza beki wa kulia na beki wa kati.
Hakika si aina ya mchezaji asiyevutia.”