Mbunge wa Gairo Ahmed Shabiby alisimama Bungeni kuchangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na mawasialiano ambapo kati ya vitu alivyoishauri serikali ni pamoja
na kuacha tabia ya kuingilia baadhi ya majukumu ya bodi inazokuwa ikiziunda kwa ajili ya utendaji.
Shabiby amesema…>>>’Hakuna watu wanafiki kama sisi baadhi yetu wabunge, miaka ya nyuma tulikuwa tunapiga kelele tunashindwa hata na nchi kama Rwanda kwa kutokuwa na ndege, leo ndege zimekuja mnasema ndege sio kipaumbele cha kwanza’ –Ahmed Shabiby
‘Mimi nasema vyote ni vipaumbele lakini viongozwe kwa mujibu wa sheria za kibiashara, mfano unaunda bodi inawataalamu alafu yanatoka maagizo ya kuingilia hiyo bodi’ –Ahmed Shabiby
‘Kutakuwa na faida gani ya kuweka bodi mpya? Kama mmeweka bodi acheni zifanye kazi zake, hakutakuwa na maana mnaweka bodi alafu mnaiingiliaingilia , acheni watu wafanye kazi zao hii ni biashara jamani’ –Ahmed Shabiby
Full video nimekuwekea hapa chini tayari…
VIDEO: Mambo 19 ya Mbunge Serukamba kumuhusu Rais Magufuli
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo