Leo July 29, 2019 nakusogezea stori kutoka +254 Kenya ambapo kuna kundi la akina dada watupu ambao wanaendesha pikipiki, wanaojiita The Inked Sisterhood, mara nyingi huwashangaza watu katika eneo walilopo.
Kundi hilo hivi karibuni lilikamilisha safari ya 270km kutoka Mji Mkuu Nairobi, kuelekea kusini katika Mji wa Loitokitok Kenya. wadada hawa uvaa viatu vya ngozi nyeusi, makoti na helmenti kichwani ndio huwakinga na madhara mbalimbali.
Baadhi ya wakazi katika Mji huo, ulio mpakani na Tanzania, walishangaa, lakini wanawake hawa wamezoea watu kuwashangaa.
Patience Mehta ambaye picha yake hiyo hapo juu, ni mkulima na msimamizi alianzisha kundi la the Inked Sisterhood miaka miwili iliyopita kama njia ya kuwaunganisha na kuwapa nguvu wanawake wanaoendesha pikipiki.
Kundi lilitokana na shule ya mafunzo ya uendeshaji pikipiki Inked Bikers training school mjini Nairobi, ambako wanawake wengi walijifunza kuendesha na hivi sasa lina wafuasi 46.
Amepewa jina la utani “Empress Peanut” kutokana na umbo lake dogo na uongozi unaovutia, Mehta alipata mshawasha wa kujifunza uendeshaji pikpiki baada ya kutazama filamu ya Nikita, ambayo nyota wake aliendesha pikipiki akiwa amevalia mavazi ya ngozi nyeusi.
Pikipiki hutumika sana kwa usafiri Mjini Nairobi, Bodaboda zimejaa mjini lakini baadhi ya watu hawavutiwi na tabia za baadhi ya madereva na kuhofia usalama wao, wengine wakiwanyanyasa wanawake
The Inked Sisterhood hukutana kila baada ya miezi michache na kuendesha pikipiki pamoja, Safari yao inayofuata ni ya 56km kuelekea Mji mdogo wa Kimende, Kaskazini mwa Mji Mkuu Nairobi.