Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Beatrice Kwayu kwa tuhuma za kumuua Evagro Msele ambaye ni mume wake kwa kutumia kitu chenye ncha kali mgongoni wakati alipokuwa akitoka nyumbani kwa mke Mdogo katika kata ya Kiruo Vunjo Mashariki
Philip Msele ndugu wa marehemu amesema baada ya mke Mkubwa Betrice kubaini kuwa marehemu alikuwa na mke mdogo alimvizia nakumchoma na kitu chenye ncha kali nyumbani kwa mke huyo mdogo na sio kwamba alifumania kama ilivyodaiwa
Kamanda wa polisi Mkoani Kilimanjaro Saimon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema kwamba mwanamke huyo anashikiliwa kwa uchunguzi zaidi