Katika kukuza sekta ya michezo Tanzania, Taasisi ya Bega kwa Bega imezindua Rede Cup kwa lengo la kutimiza ndoto za vijana wa Kitanzania wenye vipaji mbalimbali.
Salum Viduka ambaye ni Mratibu wa Matukio kutoka Taasisi ya Bega kwa Bega na Mama amesema…”Kama nilivyoeleza hapo awali huu mpango wa Dr.Samia Suluhu Cup Viwanjani ni endelevu utakaokwenda kugusa michezo yote kwahiyo taasisi yetu ya Bega kwa Bega baada ya kuona Rais anafanya kazi kubwa tukaona tuje na mpango huu endelevu unaolega kuiambia jamii juu ya michezo,”.
“Lakini mpango huu umeanzia kwenye mashindano ya mchezo wa Rede ambayo tunazindua tarehe 1 ikiwemo Sodo, Mpira wa Miguu na Mpira wa Makaratasi, Ngumi na wasanii chipukizi,”.
“Vijana ni wengi wana malengo makubwa ya michezo na sanaa, hivyo taasisi ya Bega kwa Bega tunaenda kutimiza ndoto za malengo ya vijana wa Kitanzania,”
Kwa upande wake Farida Ibuni ambaye ni Mjumbe wa Uratibu wa Taasisi ya Bega kwa Bega amesema “Tutaanza na mchezo wa Rede napenda kuwapa hamasa mchezo unapendwa na wadada na wamama nawqkqribisha CCM Mwijuma hakuna kiingilio, kila mtu anakaribishwa kuja kujifunza,”