Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta hapa nchini ambapo bei za rejareja na jumla za mafuta ya petrol, dizeli na mafuta ya taa yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es salaam zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la February 2 2022 ambapo kwa mwezi March bei za rejareja za petroli na dizeli zimeongezeka kwa Tsh. 60 kwa Lita ( sawa na 2.42%) na Tsh. 65 kwa lita (sawa na 2.77%) na mafuta ya taa imepungua kwa Tsh. 83 kwa lita (sawa na 3.63%).
EWURA imesema kuwa bei hizi zingeweza kuwa juu zaidi kama Serikali isingechukua hatua ya kuahirisha tozo ya Tsh. 100 kwa lita kwenye bidhaa za mafuta ya petrol, dizeli na mafuta ya taa.
“Kwa March 2022 bei za jumla na rejareja kwa mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara) zimeongezeka ikilinganishwa na bei zilizotolewa February 02, 2022, kwa March bei za rejareja za petroli na dizeli zimeongezeka kwa Tsh. 165/lita (sawa na 6.88% ) na Tsh. 207 kwa lita (sawa na 9.09% )
Imeelezwa kuwa mabadiilko haya ya bei yanachangiwa na kubadilika kwa bei za mafuta katika Soko la Dunia, gharama za usafirishaji na thamani ya shilingi ukilinganisha na dola ya Kimarekani.