Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta nchini ambazo zimeongezeka, ikilinganishwa na mwezi uliopita.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Godfrey Chibulunje amebainisha kuwa, bei hizo mpya zitaanza kutumika kuanzia Septemba 04, 2020. Petroli imeongezeka kwa Tsh. 20 kwa lita, Dizeli Tsh. 8 kwa lita na mafuta ya taa Tsh. 124 kwa lita.
Mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la ndani, yanatokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia, gharama za usafirishaji na gharama za ucheleweshaji wa ushushaji wa mafuta.