Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli nchini Kenya (EPRA) imetangaza kupanda kwa bei ya mafuta kwa Ksh. 9 (Tsh. 178.47) katika ukaguzi wake wa kila mwezi.
Kwa muda wa mwezi mmoja ujao lita moja ya petroli jijini Nairobi itagharimu Ksh.159.12 ( Tsh. 3,160.70), dizeli Ksh. 140 (Tsh 2,785.65) na mafuta ya taa Ksh. 127.94 (Tsh. 2,541.35).
EPRA imesema Serikali itatumia Hazina ya Maendeleo ya Petroli (PDL) kuwaepusha Wananchi na bei hizo za juu huku madereva wa Nairobi wakilipa Ksh. 159.12 (Tsh 3,160.70) kwa lita moja ya petroli, bei halisi ni Ksh.184.68 (Tsh.3,668.41) kumaanisha kuwa Serikali italipa Ksh.25.76 (Tsh. 511.69) kama ruzuku .
Serikali imetangaza kwamba ruzuku ya dizeli ni Ksh. 48.19 (Tsh. 957.23) kwa lita huku ile ya mafuta ya taa ikiwa ni Ksh. 42.43 (Tsh.957.23) kwa lita ambapo bei hizi zinajumuisha kodi.