Beki wa kulia wa Bayern Munich Sacha Boey atakuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa baada ya kupata jeraha lingine akiwa mazoezini.
Akiwa amerejea hivi majuzi kutoka kwa muda wa kukaa nje ya uwanja, Sascha Boey amepata pigo jipya la jeraha.
Bayern Munich wamethibitisha kuwa beki huyo wa kulia amechanika misuli kwenye uwanja wa mazoezi.
Kwa mujibu wa Bild, jeraha hilo litamfanya Mfaransa huyo kuwa nje ya uwanja kwa wiki sita.
Bayern walitumia euro milioni 30 kumnunua Boey kutoka Galatasaray mwezi Januari.
Tangu wakati huo, amecheza mechi mbili pekee kwenye Bundesliga.