Beki huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Nottingham Forest ya Ligi Kuu ya Uingereza akitokea klabu ya La Liga ya Sevilla, anashtakiwa kwa kumnyanyasa kingono mwanamitindo kwenye sherehe yake ya kuzaliwa Januari 1, 2019.
Kulingana na kituo cha habari cha Argentina TN, Montiel. anatarajiwa kuhudhuria korti katika jiji la San Justo mnamo Septemba 17 na 20.
Montiel, ambaye alifunga penalti ya ushindi kwa Argentina katika fainali ya Kombe la Dunia 2022, amewekwa chini ya uchunguzi rasmi – pamoja na rafiki yake Alexis Acosta – na inasemekana aliamriwa kufanyiwa vipimo vya akili mnamo Septemba 2 na 5.
Mshtaki wa Montiel anadai kuwa alipewa dawa za kulevya na kubakwa kabla ya kutishiwa na jamaa na washirika wa mshtakiwa.
Mshtaki anaripotiwa kuwa aliomba uchunguzi wa kiakili ufanyike kwa sababu ya “makosa” yanayodaiwa katika kesi hiyo.
Montiel alitoa ushahidi wake kwa hiari mbele ya jaji mwaka jana na anadumisha kutokuwa na hatia.
Waendesha mashtaka bado hawajawasilisha mashtaka yoyote na hakuna taarifa rasmi ikiwa kesi hiyo itasikilizwa.