Kwenye gazeti la Mwanaspoti, Kaze ambaye kwa sasa anaitumikia Vital’O ya kwao Burundi, alisema hakushangazwa na maamuzi ya klabu hiyo ya kumtimua Loga ambapo kwake kilichomshtua ni juu ya uamuzi huo kuchelewa kufanyika.
Kaze alisema Loga hakuwa kocha mzuri ndani na nje ya timu akidai alichangia kwa kiasi kikubwa kushusha kasi ya maendeleo ya wachezaji, alikuwa mkorofi kwa wachezaji wake jambo ambalo liliweka tabaka kubwa kati yake na wachezaji ambapo hakuna mchezaji aliyekuwa akifurahia uwepo wa kocha huyo mwenye mikwara mingi.
“Sishangai kusikia Loga ametimuliwa, walitakiwa kufanya hivyo mapema sana na ni bahati mbaya hakukuwa na mchezaji aliyekuwa tayari kusema hilo mapema, hakuna mchezaji hata mmoja ambaye alikuwa akifurahia maisha na Loga, kila alipokuja mazoezini na hata katika mechi watu tulikosa raha.”