Mwimbaji Staa wa Bongofleva, Ben Pol ameomba radhi kwa maneno aliyoyasema kuhusu ndoa yake wakati wa mfululizo wa mahojiano yake maalumu na Mtangazaji MillardAyo, yaliyoanza kutangazwa tarehe 13 Januari, 2023.
“Nia yangu haikuwa kuumiza bali kuwashirikisha juu ya uzoefu wangu ndani ya ndoa na nitalibeba jukumu hili kikamilifu, pia nilitaka kueleza jinsi ilivyoathiri afya yangu ya akili, hata hivyo, ninatambua kwamba maneno yangu yalimuumiza Mke wangu wa zamani na ninaomba msamaha kwake na kwa umma”
“Ingawa ninataka kuendelea kuzungumza juu ya afya ya akili na kuzungumza juu ya uzoefu wangu, nitajitahidi kufanya hivyo kwa njia ambayo ni bora zaidi na yenye kujenga zaidi”
Itakumbukwa akihojiwa na Millard Ayo, Frida Amani wa Vido Vidox wa AMPLIFAYA ya Clouds FM alisema hakuifurahia ndoa yake kama alivyotarajia na kukiri kuwa hali ilikua tofauti na jinsi Watu wengi kwa nje walivyokuwa waki-imagine kupitia picha mbalimbali alizokuwa akiziweka mtandaoni.
Kwa mara ya kwanza Ben Pol alifunguka kuhusu maisha yake ya ndoa na sababu kuu iliyoivunja na kusema haku-enjoy matunda ya ndoa kama alivyoziona ndoa nyingine “yani sisi sanasana naweza nikasema ilikua ni kaa hapo upige picha, paaa paa weka nini……. sisemi kwa ubaya na wala sipo hapa kwa ajili ya kumpeleka Mtu mwingine chini ila tu kwa mtazamo wangu mimi naona kama niliingia kwenye picha kuleta ule ukamilifu”