Beki wa Manchester City Benjamin Mendy ameongezewa shitaka moja la ubakaji na sasa yamefikia saba dhidi ya wadada wa watano wenye umri zaidi ya miaka 16.
Mlalamikaji huyo wa mwisho amedai tukio hilo limetokea Julai mwaka huu, huku mengine sita ya awali yakidaiwa kutokea kati ya Oktoba 2020 na Agosti 2021 katika Jumba lake la kifahari jijini Manchester.
Mendy bado anaendelea kuwepo mahabusu ya polisi tangu Agosti mwaka huu alipofunguliwa mashitaka hayo na kesi yake inataraji kusikilizwa mwakani Januari.