Rais Cyril Ramaphosa ameondolewa “makosa yoyote” katika uchunguzi uliofanywa na Benki Kuu ya Afrika Kusini (SARB) kuhusu fedha za kigeni ambazo hazijatangazwa kutoka shamba lake la Phala Phala katika jimbo la Limpopo miaka mitatu iliyopita, gavana wa SARB Lesetja Kganyago amesema.
Kulingana na habari, nyaraka na ushahidi uliokusanywa wakati wa uchunguzi, benki kuu ilihitimisha kuwa hakukuwa na “muamala kamilifu,” gavana alisema katika taarifa Jumatatu.
Kutokana na hili, SARB haikuweza kuthibitisha kwamba kulikuwa na ukiukwaji wowote wa Kanuni za Udhibiti wa Ubadilishanaji Fedha (haswa Kanuni ya 6(1)) na Ntaba Nyoni Estates CC, taasisi inayohusika, au rais mwenyewe, Kganyago alisema.
Ilifahamika kwamba Ramaphosa alikuwa ameficha dola takribani milioni 4 ndani ya sofa.
Wakati wa uchunguzi, Rais huyo alijichanganya mwenyewe kuhusu chanzo cha fedha hizo.
Lakini baadae alikiri kupokea mamilioni ya Dola mwaka 2019 baada ya kuuza Nyati 20 kwa mfanyabiashara wa Sudan.