Amerika Kaskazini kwa upande wake imeingiza vyuo vingi zaidi kwenye list hii. Na inaelezwa kuwa kwa takribani miaka 12 hakukuwahi kuwa na chuo chochote kutoka nje ya Marekani kilichofanikiwa kuingia kwenye top 10 ya vyuo.

Inatajwa kuwa kwa mwaka huu 2016, Marekani pekee imeingiza vyuo vikuu bora 148, huku vyuo 63 vikiwa kwenye list ya top 200.

http://uopnews.port.ac.uk/wp-content/uploads/2012/10/THE_WUR_TOP_4001.jpg

Bara la Ulaya

United Kingdom, imeingiza vyuo 91, wakati nchi za Ujerumani, Italy, Ufaransa na Hispania zina jumla ya vyuo 26 kwenye list. na kwa mujibu wa Times Higher Education notes, Bara la Ulaya limeanza kushuka nafasi zake na kupitwa na nchi za bara la Asia.

Bara la Asia

Bara la Asia limeingiza jumla ya vyuo 289 kutoka nchi 24, na vyuo 19 viko kwenye list ya top 200, ikiwa imepanda kutoka nchi 15 mwaka 2015. Nchi nyingine kama Singapore, China, Japan, Hong Kong na Netherlands pia zimetajwa kuwa na vyuo vikuu venye elimu bora zaidi duniani.

ULIPITWA NA TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU GARI LA MWANAJESHI LILILOIBIWA LIKIWA NA MTOTO NDANI? TAZAMA HAPA