Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) imesema mchango wa Sekta hiyo katika mapato ya Serikali umeongezeka ambapo kodi iliyokusanywa na Serikali imeongezeka kutoka Tsh. bilioni 33.6 mwaka 2016/17 hadi kufikia Tsh. bilioni 170.4 mwaka 2022/23.
“Kiwango hicho ni ongezeko la wastani wa 407.1% kwa mwaka katika kipindi hicho”
Bodi hiyo pia imesema Tanzania imefanikiwa kuzalisha ajira zilizo rasmi na zisizo rasmi (direct and indirect employment)
zipatazo zaidi ya 25,000 hivyo Sekta hii imefanikiwa kutoa mchango mkubwa katika uzalishaji wa ajira Nchini.
“Mapato ya Serikali yatokanayo na Kodi ya biashara ya michezo ya kubahatisha yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka
kama ilivyokwisha elezwa.
“Tanzania imekuwa mfano kwa baadhi ya Nchi za Afrika, hususani Ukanda wa Mashariki, Kati na Kusini ukiondoa Afrika Kusini”
“Tanzania imekuwa Mwalimu kwa baadhi ya Nchi zikiwemo Kenya, Uganda, Zimbabwe, Malawi na Ethiopia”