Kutoka nchini Kenya, kuna taarifa za polisi katika Mji wa Bomet kumshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za kumjeruhi vibaya baba yake kwa kumchoma moto.
Baba huyo ambaye ana umri wa miaka 55, ameeleza polisi kuwa mwanaye huyo alimkuta akiwa kwenye kioski cha familia yao akiwa anakula na kijana huyo kuanza kumwagia kitu alichohisi kuwa ni petroli na baadaye kumuwasha moto.
Afisa wa Polisi Samson Rukunga ameeleza kuwa mzee huyu amejeruhiwa vibaya na alikimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
Polisi hadi sasa bado hawajaeleza sababu ya kijana huyo ya kumchoma moto baba yake mzazi
Mazungumzo Rais Magufuli na Afande Sele “chapa kazi”