Leo April 13, 2018 Shirika la Mabasi yaendayo Haraka DSM (UDART), limesema kuanzia sasa mfumo wa ukusanyaji nauli wa shirika hilo utakuwa chini ya TTCL badala ya kampuni ya Maxcom.
Akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko hayo, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano, UDART, Deus Bugaywa amesema mkataba baina ya UDART na Maxcom umeisha.
Bugaywa amesema mkataba wa Maxcom umemalizika baada ya kudumu nao kwa miaka 2, ambapo wameamua kusaini mkataba mwingine na TTCL.
“Sababu kubwa ni kwamba tumemaliza mkataba nao, hii ni kawaida kama ilivyo kwa kampuni zinavyofanya, ambapo tumempata mbia mpya ambaye ni TTCL,” -Bugaywa.
Pia Bugaywa amesema kuwa mabadiliko hayo yanaweza kusababisha usumbufu katika siku chache kuanzia sasa kutokana mfumo huo mpya wa TTCL.
“Nawaomba watumiaji wa usafiri huu wawe na imani kwani tunaamini mabadiliko haya yatakuwa ya kisasa,” -Bugaywa.