Leo Dec 21 2017 Manispaa ya K’ndoni imeendelea kutekeleza maagizo ya kubomoa sehemu za wazi ambazo zimevamiwa na wananchi. Katibu Tawala wa manispaa ya Kinondoni Gift Msuya ameeleza zoezi hilo la bomoa bomoa lilipoanzia na ametoa rai kama kuna yoyote amelipa kodi Manispaa kwa ajili ya kutumia maeneo hayo wako tayari kulipa fidia.
“Napenda kusema tu jambo moja hii operseheni ni endelevu, tutapita kama umejenga kinyume cha sheria tutakuondoa, tunapenda tutume ujumbe maeneo mengine ya DSM tunapenda kuona maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya huduma za jamii yaachwe kama ilivyoainishwa,” -Katibu Tawala Gift Msuya