Baada ya baadhi ya wabunge wa upinzani kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa muda tofauti kwa madai ya kukiuka kanuni za bunge.
Leo June 17 2016 idadi ya wabunge kusimamishwa imeongezeka baada ya Naibu Spika, Tulia Ackson kutangaza kusimamishwa kwa wabunge wawili ambao ni Mbunge wa viti Maalum CHADEMA Suzan Lyimo na Anatropia Theonest.
Mbunge Suzan Lyimo amesimamishwa na Bunge kuhudhuria vikao vitano vya Bunge baada ya kubainika kusema uongo kwamba Jeshi la polisi nchini limenunua magari 777 ya washawasha wakati ukweli ni kwamba hiyo ni Idadi ya magari inayopangwa kuingizwa na jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Licha ya Mbunge kuonesha ushirikiano kwa kamati ya maadili, haki na madaraka ya bunge, kamati imemwona Mbunge ni mzoefu wa shughuli za bunge hivyo anapaswa kusimamishwa vikao hivyo kuanzia June 17 hadi 24 mwaka huu.
Aidha Mbunge Anatropia Theonest amesimamishwa kuhudhuria vikao vitatu vya bunge kwa kosa la kulidanganya Bunge kuwa waziri wa ardhi na nyumba William Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
Mbunge wa viti maalum CHADEMA Susan Lymo amesimamishwa kuhudhuria vikao vitano kwa kosa la kulidanganya bunge pic.twitter.com/uPTpLgQDfd
— millardayo (@millardayo) June 17, 2016
#MillardAyoUPDATES Mbunge Suzan Lyimo amesimamishwa vikao baada ya kudanganya Bunge kuwa Jeshi la polisi limenunua magari 777 ya washawasha
— millardayo (@millardayo) June 17, 2016
Mbunge Anatropia Theonest kasimamishwa kuhudhuri vikao 3 kwa kudanganya kuwa Waziri Lukuvi alichukua ardhi ya wanchi pic.twitter.com/NOMpp6W2yC
— millardayo (@millardayo) June 17, 2016
ULIKOSA YALIYOMKUTA MBUNGE ALIYESEMA DK. MWAKYEMBE NI JIBU? BONYEZA PLAY HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE