Timu ya taifa ya Congo baada ya kupokea kipigo cha magoli 2-0 kutoka timu ya taifa ya Uganda, wengi walishitushwa kuona Congo ikiwa na mastaa wake vile imekubali kufungwa na Uganda na kuzidiwa kimchezo, baada ya mchezo tulifanikiwa kumpata kocha msaidizi wa Congo DRC Mwinyi Zahera.
Zahera amejitetea kuwa sababu iliyopelekea wao wakafungwa ni uchovu ambao wameupata siku moja kabla ya mchezo, Zahera anaeleza walivyokuwa kambini Hispania waliwanyia vipimo wachezaji wao na kuvituma CAF lakini jana CAF wakawachukua wachezaji wa Congo toka saa tano asubuhi hadi saa nne usiku wakiwapima tu.
“Tatizo linatokana na kilichotokea jana unasikia jana tunapata habari asubuhi ya kusema kwamba CAF, Sisi tulikuwa mazoezini Hispania tulifanya vipimo vyote wakatuma CAF kisha jana asubuhi CAF wanatuambia kuna tatizo ya vile vipimo tulivyotuma wakarudisha wachezaji wakaenda saa tano hadi saa nne ya usiku”>>>Zahera
VIDEO: Okwi baada ya kukabidhiwa tuzo AFCON 2019