Good news ikufikiea kuwa wakati tukiwa tunaisubiria club ya Everton ya England kuja Dar es Salaam Tanzania kwa mara ya kwanza katika historia July 13 kucheza mechi ya kirafiki na Bingwa wa SportPesa Super Cup Gor Mahia ya Kenya, leo June 20 wametoa ratiba yao.
Everton leo June 20 2017 imetoa ratiba yake ya maandalizi ya msimu mpya wa 2017/2018, Everton wametoa ratiba yao ambapo baada ya kucheza Gor Mahia July 13 uwanja wa Taifa Dar es Salaam watasafiri hadi Uholanzi kucheza na FC Twente game ya kirafiki July 19.
Baada ya game hizo mbili July 22 2017 watakuwa Ubelgiji katika uwanja wa Luminus Arena kucheza dhidi ya timu ya KRC Genk ya Ubelgiji, timu ambayo inachezewa na mtanzania Mbwana Samatta na watacheza katika uwanja wa nyumbani wa KRC Genk.
Unachotakiwa kufahamu ni kuwa Everton ambapo wanakuja Tanzania kucheza na Bingwa wa SportPesa Super Cup ambao ni Gor Mahia kutoka Kenya watakuja na wachezaji wake wote wa kikosi cha kwanza, kwa sababu kocha wao Ronald Koeman amesema hazichukulii poa game za maandalizi ya msimu.
VIDEO: All Goals Taifa Stars vs Lesotho June 10 2017, Full Time 1-1