Leo February 23, 2018 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni ameeleza kuwa kukamata waendesha pikipiki wenye makosa barabarani huwa ni hatari hivyo maaskari wa usalama barabarani hutumia namba zake za usajili kuwatafuta.
Hatahivyo ameeleza kuwa wale ambao wananunua usajili kwa pamoja wamekuwa hawabadilishi usajili, hivyo askari anaweza kumkamata mtu wa pikipiki lakini akienda kuangalia kwenye rekodi za usajili anakuta bado liko jina la mmiliki.
Kutokana na suala hilo Masauni ametoa agizo la kukamatwa na kuwekwa mahabusu na kisha kupelekwa mahakamani wamiliki wa pikipiki ambao wameuza pikipiki bila kubadili usajili wake wa umiliki.
“Tutafanya hivi hadi hapo desturi hii ya kuuza pikipiki bila kubadilisha usajili husika itakapokoma, kila anayeendesha pikipiki awe na usajili wa mmiliki kwa wakati huo ili atakapofanya kosa tujue namna ya kumdhibiti na kumshughulikia kwa mujibu wa sheria.” – Naibu Waziri Masauni
Kilichosababisha Kesi ya Tido Mhando kuahirishwa
Rais Magufuli na Kenyatta wamewaagiza Mawaziri kutatua tofauti ndogondogo zilizopo