Neno ‘Baharia’ limeanza kutumika muda mrefu sana lakini siku za hivi karibuni limeonekana kushika kasi na kutumiwa sana mitaani na mitandaoni huku kila mmoja akilitumia kwa style yake iwe kwenye mazungumzo ya kawaida au ya utani.
Lakini bado maswali ni mengi kuhusu maana halisi ya Baharia na sifa za yule anayefaa kuitwa Baharia.
Kupitia AyoTV na ‘millardayo.com’ tunae Katibu Mkuu wa Chama cha Mabaharia Tanzania Capt. Josiah Mwakibuja ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya kusaidia Matatizo ya Mabaharia Afrika na Katibu wa Bodi ya kutoa misaada kwa Mabaharia.