Reporter wa AyoTV na millardayo.com ameripoti kutokea mtaa wa Rwamishenye manispaa ya Bukoba kwamba limetokea tetemeko. Amesema tetemeko hilo ambalo limetokea mida ya saa saba na nusu usiku huu wa kuamkia April 30, lilidumu kwa sekunde zisizozidi 15.
Mpaka sasa anazunguka kwenye mitaa mbalimbali na anachoshuhudia ni Watu mbalimbali waliotoka nje ya nyumba zao kuhofia tetemeko jingine. Hakuna madhara yoyote yaliyoripotiwa mpaka sasa lakini AyoTV na millardayo.com zinaendelea kufatilia kwa ukaribu.
Hakikisha umejiunga na APP ya ‘millardayo’ pia Twitter FB na Instagram zenye jina la ‘millardayo’ ili kila breaking news ikufikie kwa wakati.
#BREAKING Wengi wa Wakazi wa Bukoba wako nje ya nyumba kwa hofu baada ya tetemeko usiku huu, https://t.co/G3BpafI2ae na AyoTV zinafatilia.
— millard ayo (@millardayo) April 29, 2017
#BREAKING Reporter wa AyoTV & https://t.co/G3BpafI2ae Bukoba Kagera anasema limetokea tetemeko usiku huu, limedumu karibu sekunde 15.
— millard ayo (@millardayo) April 29, 2017
VIDEO: Waziri Mbarawa alivyosimamishwa kujibu ahadi ya meli Bukoba