Jumapili ya November 13 2016 timu ya taifa ya Zimbabwe ambayo inajiandaa na michuano ya AFCON 2017 Gabon, itacheza mchezo wa kirafiki uliokuwa katika kalenda ya FIFA dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, Zimbabwe ambayo ipo Kundi B lenye timu za Senegal, Tunisia na Algeria AFCON, imeita kikosi cha wachezaji 23 kupambana na Tanzania.
1-Katika list ya wachezaji 23 walioitwa kucheza dhidi ya Tanzania, ni wachezaji 8 ndio wanaocheza Ligi ya nyumbani.
2- Zimbabwe wana mshambuliaji anayeongoza msimamo wa wafungaji katika Ligi Kuu Afrika ya Kusini ABSA Tendai Ndoro hiyo ni kwa mujibu wa gazeti la The Saturday Herald la hapa Zimbabwe.
3- Zimbabwe pia wanamchezaji anayecheza Ligi moja na nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta, mshambuliaji wao Knowledge Musona ndio mchezaji anayecheza klabu ya KV Oostende ya Ligi Kuu Ubelgiji.
4- Kwa mujibu wa moja kati ya mashabiki wa soka Zimbabwe Khama Billiat aliyetoka kushinda klabu bingwa Afrika na Mamelodi Sundowns ndio mchezaji hatari au nyota wa kikosi cha Zimbabwe Warriors.
5-Khama Billiat ni miongoni wa wachezaji walioteuliwa katika list ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi ya ndani ya Afrika, tuzo ambayo mwaka 2015 ilichukuliwa na Samatta.
6- Katika viwango vya soka vya FIFA Tanzania ipo nafasi ya 144 wakati Zimbabwe ipo nafasi ya 110.
7- Kikosi kamili cha wachezaji 23 wa Zimbabwe walioitwa kucheza dhidi ya Taifa Stars
MAGOLIKIPA: Donovan Bernard (How Mine), Tatenda Mukuruva (Dynamos), Nelson Chadya (Ngezi Platinum)
MABEKI: Onismor Bhasera (Super Sport United), Hardlife Zvirekwi (CAPS United), Bruce Kangwa (Azam FC), Lawrence Mhlanga (Chiken Inn), Teenage Hadebe (Chiken Inn), Tendai Ndlovu (Highlanders), Oscar Machapa (AS Vita Club)
VIUNGO: Willard Katsande (Kaizer Chiefs), Marvelous Nakamba (Vitesse Arnhem), Marshall Mudehwe (FC Platinum), Raphael Kutinyu (Chiken Inn), Danny Phiri (Golden Arrows), Kudakwashe Mahachi (Golden Arrows), Khama Billiat (Mamelodi Sundowns).
WASHAMBULIAJI: Knowledge Musona (KV Oostende), Mathew Rusike (Helsingborgs IF), Tendai Ndoro (Orlando Pirates), Cuthbert Malajila (Bidvest Wits), Philana Kadewere (Djurgardens IF), Nyasha Mushekwi (Dalian Yifang)
ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0