Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, wamekubaliana kuongeza matumizi ya fedha za nchi badala ya za kigeni kwenye biashara kati ya Tanzania na India.
Hatua hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya dola za Marekani kwenye nchi hizo kwa sababu kwa sasa (kwa takwimu za India 2022/23) thamani ya biashara ya India na Tanzania imefika dola bilioni 6.7 (zaidi ya shilingi trilioni 14) – ongezeko kubwa kutoka dola bilioni 3.2 mwaka 2021/22 (takwimu za Tanzania).
Wakizungumza katika mkutano wa pamoja na Waandishi wa habari baada ya mazungumzo yao ya faragha, Waziri Mkuu Modi amesema lengo la hatua hiyo ni kuongeza biashara na kupunguza gharama.