Rais wa Marekani Joe Biden na timu yake wanaweza kutangaza wiki ijayo kwa njia ya video hatua yake ya kuwania muhula mwengine kwenye uchaguzi wa 2024,na itajiri baada ya miaka minne tangu siku ya uzinduzi wa kampeni yake ya mwaka wa 2020 hata hivyo, chanzo hicho kimesema kuwa muda kamili wa tangazo hilo unaweza kubadilika.
Washauri wa Biden wameongeza kasi ya mipango ya uzinduzi ulioatarajiwa kwa muda mrefu wa azma ya rais kwa muhula wa pili wa miaka minne, hapo mwaka wa 2024.
Wiki iliyopita, Biden alisema atazindua kampeni yake “hivi karibuni.”
White House haikujibu mara moja ombi la Reuters la kutoa maelezo, huku kamati ya kitaifa ya chama cha Democratic ikijizuia kutoa kauli.
Biden alisema kwa muda mrefu kuwa ana nia ya kugombea tena lakini kutotangaza rasmi kumezua mashaka miongoni mwa wafuasi wake kuhusu iwapo mmoja wa viongozi wakongwe duniani anaweza kuamua kuwania muhula mwengine wa miaka minne na iwapo atagombea urais na kushinda, Biden atakuwa na umri wa miaka 86 mwishoni mwa muhula wake wa pili.
Anatarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki ijayo na wachangishaji wa fedha wa kujitolea kutoka timu yake ya kampeni ya mwaka wa 2020 chanzo kinachofahamu suala hilo kimesema Alhamisi.