Twitter imethibitisha kwamba Mamilioni ya wafuasi wa akaunti rasmi ya rais wa Marekani watafutwa kabla ya akaunti hiyo kukabidhiwa utawala wa rais mteule, Joe Biden.
Timu ya Biden ‘ilipinga mpango huo lakini kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii ilisema kwamba uamuzi wake ‘haubadiliki’, hatua hiyo inaashiria mabadiliko kutoka kwa utawala unaoondoka madaralani.
Twitter ilikubali ombi la Rais Donald Trump mwaka 2016 kuwarithi Mamilioni ya wafuasi wa, Barrck Obama.
”Mwaka 2016, utawala wa rais Trump uliwarithi wafuasi wote wa rais Obama katika akaunti ya POTUS na ile ya Whitehouse”, Rob Flaherty, Mkurugenzi wa masuala ya mtandaoni amesema katika ujumbe wake wa Twitter siku ya Jumatatu.