White House imetangaza Alhamisi kwamba Rais wa Marekani Joe Biden, Septemba 26 atafanya mazungumzo kwenye Ikulu hiyo na mwenzake wa Ukraine Volodymr Zelenskyy, kuhusu vita vinavyoendelea kati ya taifa lake la Russia.
Taarifa kutoka kwa msemaji wa White House Karine Jean Pierre, imesema kuwa Zelenskyy kwenye kikao hicho pia atakutana na Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris.
Biden na Harris wanatarajiwa kuhimiza msimamo wao usiotikisika wa kusimama na Ukraine hadi pale itakaposhinda vita hivyo, Jean Pierre ameongeza kusema.
Zelenskyy kwa upande wake amesema kuwa ana mpango wa kushinda vita hivyo dhidi ya Russia, na kwamba atamueleza Biden kuhusu pendekezo lake.
Katika wiki za karibuni, Zelenskyy ameeleza kuvunjika moyo kutokana na kutopewa idhini na washirika wake hasa Marekani na Uingereza, kutumia silaha za masafa marefu dhidi ya malengo ndani ya Russia.
Hata hivyo mataifa hayo yanaonekana kujiepusha kuhusika kwenye vita hivyo moja kwa moja