Furaha iliyoonyeshwa na 50 Cent katika matatizo anayopitia staa wa muziki Sean ‘Diddy’ Combs huenda ikachochewa na wivu wa kimapenzi, baada ya Combs kushutumiwa kwa kumlipa ex wa 50 Cent kwa kutoa huduma za ngono.
Dunia ilipokea kwa mshtuko mkubwa sakata zima la rapper P Diddy pindi ambapo nyumba zake zilizopo jijini Miami pamoja na Los Angeles zilipovamiwa na maafisa wa usalama mwanzoni mwa wiki hii kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea wa biashara za ngono anazoshtumiwa kufanya.
Sakata zima lilichangamka zaidi baada ya maoni ya rapper 50 Cents kumtupia maneno ya kukejeli kwenye mitandao ya kijamii na ofcourse jambo hili lilienda viral … ambapo 50 cents alionyesha kucomment kwenye page mbali mbali mitandaoni zikionyesha kufurahishwa kwa kitendo cha rapper Diddy kupatwa na matatizo.
Mapema hii leo, mapya haya yaliyoibuka kuwa Combs mwenye umri wa miaka 54 ametuhumiwa kumlipa mshahara wa kila mwezi Baby Mama wa 50 Cent aitwae Daphne kwaajili ya kutoa huduma za ngono. Yote haya yaliandikwa katika nyaraka za kesi ya mashtaka yaliyofunguliwa na aliyekuwa producer wa P Diddy Rodney Jones akidai kuwa Ex wake 50 cents alikuwa mfanyakazi wake Diddy na alikuwa akitoa huduma hizo.
Mashtaka hayo yameandikwa katika nyaraka zenye kurasa 73 iliyowasilishwa na Rodney Jones, mmoja wa Ma-Producer wa Sean ‘Diddy’ Combs, ambaye anadai kuwa Combs alimuweka alikuwa akimpapasa na kumgusa mara kwa mara bila kuombwa ridhaa yake, alituhumu kwa unyanyasaji wa kijinsia na kuomba fida ya dola milioni 30 (Tzs Bil 77) akiongeza kuwa aliamriwa kufanya ngono na wafanyakazi wa huduma hizo mbele ya Staa Diddy na kusema anaushahidi wa video zinazoonyesha mambo anayoyafanya Sean ‘Diddy’ Combs, kati ya mwaka 2022 na 2023, pia alidai kuwa wasichana wadogo walihusishwa na biashara hiyo ya ngono.