Mbali na kwamba Joseph Kusaga amewafungulia Dunia vijana wengi wa kitanzania lakini leo hii nakukutanisha na Makili ambae nae anarekodi zake mbalimbali za utafutaji wa maisha na mpaka kumiliki Radio Station Mkoani Arusha.
Julius Makiri Jenge ni Kijana wa Kitanzania ambae kujiweka kwake karibu na Big Joe Joseph Kusaga kumefanya kufanikisha kile kinachomuhemisha Mkoani Arusha.
Leo hii amekaa kwenye Millardayo.com kueleza yale ambayo yapo nyuma ya pazia kuhusu ukaribu wake na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga na mengineyo tusiyoyajua.
‘Kiukweli Joseph Kusaga kwangu ni zaidi ya kaka unajua miaka ya 90’s wakati nasoma Pale Shaaban Robert enzi zile sisi tulikuwa tunaenda kwenye Disco ambayo alikuwa akipiga nyimbo tofauti si unajua ujana na Kusaga ndie alikuwa mtu pekee mwenye kushawishi enzi hizo masuala ya burudani’- Julius Makiri Jenge
‘Na yeye alikuwa ni mtu wa kukataa kushindwa katika kile anachokipambania na wakati wa 90’s kazitwanga sana nyimbo na hakuna mtu wa miaka hiyo ambae alikuwa hamjui Kusaga ndioe alikuwa mtu pekee akitoa burudani kwenye Disco’ – Julius Makiri Jenge
‘Sasa basi mimi baada ya kumaliza masomo nilienda Marekani Mwaka 1996 tunahitaji kujifuta na katika kujitafuta kwangu niliporudi Dar Mwaka 2000 nikajihusisha na mambo ya Recording Studio ambapo wakati huo ilikuwa ikitambulika kwa jina la Mambo Jambo Records ilifanya vizuri wakati huo’ Julius Makiri Jenge
‘Lengo la kuanzisha Mambo Jambo Records ni kukuza ndoto za vijana na kuifanya Bongo Fleva ikue zaidi enzi hizo hauwezi sema kitu kuhusu Bongo Fleva tafauti na miaka hii ya sasa ambapo mambo yamebadili ila ndio utandawazi ulivyo hauwezi sema chochote itabidi uendane na nyakati’- Julius Makiri Jenge
‘Na Mzoefu wangu Mkuu wa mambo ya burudani alikuwa ni kaka yangu Joseph Kusaga na ndiye alikuwa Mshauri wangu hivyo pale ambapo nilipokuwa nakwama namfuata na ananipa Ushauri kadhaa namna ya kufanikisha hitaji la moyo wangu’-
‘Mwaka 2002 kama sijakosea nakumbuka kuna sehemu tulikuwa tunapata chakula cha jioni na kaka yetu Joseph Kusaga kwasababu yeye ndio nuru yetu ya kupata mawazo na alikuwa si mchoyo kutoa kila alichojaaliwa lakini lazima uwe na Vision yaani Maono kwa kile unachohitaji kukifanya ndicho alikuwa akisisitiza sana sana’
‘Na Wakati alipokuwa akipata safari za Marekani Las Vegas kila Mwaka kwenye Radio and TV conference (NAB Show) ndio ulikuwa mwanzo wangu mimi kujua vitu tofauti tofauti kunifunza nyanja mbalimbali za hii tasnia ya Habari kutokea kwake’
‘Sikuwa muoga wa kujaribu kwani nilishashibishwa chakula chenye mawazo chanya kwa kaka yangu Joseph Kusaga hivyo niliamini kupitia yeye ndipo Mwaka 2004 nikaenda Wizara husika kufuatilia masuala ya vibali nijaribu pia mambo ya Radio ndipo nikafanikiwa kupata Kibali cha kurusha Matangazo ya Radio kupitia Frequence 92.9 na ndio ambayo leo hii inapasua anga na mawimbi yake kwa jina la Mega FM iliyopo Mkoani Arusha’
‘Mega Fm inasikika Arusha pia hata online kupitia https://www.megafmtz.com/ japo tuna regional license kwa mikoa 10 hivyo ni hatua kubwa siku zinazozidi kwenda nina mipango mingi mizuri’
‘Hivyo naweza kusema Joseph Kusaga amenipa moyo, Ujasiri wa kufanya yale yote ambayo nilihisi ni vugumu hususani masuala ya Radio na wala sio mchoyo kwenye ukweli atakuambia na ambapo si salama atakuambia kwahiyo ni mtu mwema ama ni Baba mwenye kutaka vijana wafanikiwe kutokana na ndoto zao kwani aligundua ndoto yangu lakini hakuwa mchoyo wa kunipa mawazo chanya juu ya kufanikisha nilichofanikisha leo hii’