Baada ya habari gumzo ya dunia leo kwamba kuna Mwanamke wa nchini Argentina amepona virusi vya ukimwi bila ya kutumia dawa wala kutibiwa likitajwa kuwa ni tukio la pili la aina hii kuwahi kutokea duniani, Dr. Isaac Maro wa TMH Health Centre Sinza ameketi na Amplifaya ya CloudsFM kueleza tukio hili ambalo hata yeye amelifatilia.
Kabla ya kusoma alichosema Dr. Maro kwanza inabidi ufahamu kwmaba Madaktari wa Argentina wanaamini kwamba kwenye tukio hili jipya mfumo wa kinga ya mwili wa mgonjwa huyo ndio ulisafisha virusi hivyo vya UKIMWI.
“Ni mara chache sana imetokea tukapata ripoti nzuri kama hii, ukweli ni kwamba huyu Mgonjwa ameonekana kufanikiwa kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kiasi ambacho kinga yake imeweza kuvipiga vizuri vya UKIMWI na kuvipoteza kabisa, huyu ni Mgonjwa wa pili kufanikiwa kama hivi, mwingine wa kwanza tulimtangaza mwaka jana” Dr. Isaac Maro
MZEE ANAISHI NA MAMBA TANZANIA, ANAONGEA NAE KAMA MTOTO WAKE, ANAMUITA “AJABU”