Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Motisun Group ambaye pia anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea nchini Tanzania na mfanyabiashara, Subhash Patel amefariki Jana Desemba 14.
Taarifa kutoka chanzo cha karibu zimeeleza kuwa, kifo hicho kimetokea mapema jana na taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
May, 2017 Patel alitajwa na Jarida la Forbes la Marekani kuwa miongoni mwa wafanyabiashara mabilionea 10, ambao wanamiliki biashara zinazoingiza kipato cha Dola za Marekani Milioni 50 au zaidi kwa mwaka.
Mwaka 1992, Subash Patel alianza kujihusisha na biashara ya mashine mbalimbali Jijini DSM.
Katika kipindi cha miongo miwili, ameigeuza biashara hiyo katika Motisun Group, himaya ya kampuni tofauti 15 katika seta za chuma, madini, plastiki, rangi, usindikaji vyakula na mali zisizohamishika.
Pia kuna hoteli za kitalii ikiwamo Sea Cliff Resort ya Zanzibar na Hotel White Sands ya jijini Dar es Salaam.