Moja ya habari iliwaacha wengi mdomo wazi wiki hii nchini Afrika Kusini ni pamoja na taarifa za kifo cha Mwanaume mwenye umri wa miaka 63 ambae polisi nchini Afrika Kusini walisema kuwa alifariki dunia kwa kujiua alitambuliwa na vyombo vya habari kama Bilionea Markus Jooste aliyekuwa CEO wa zamani wa kampuni ya Steinhoff ambae kwa mujibu wa Forbes mwaka 2015 kiwango cha utajiri wake ulifikia dola milioni 400.
Jooste, ambae alibadilisha Kampuni ya Steinhoff kutoka kuwa kampuni ndogo ya furniture jijini Johannesburg hadi kuwa muuzaji mkubwa wa bidhaa za rejareja kwenye safu za kimataifa, alipigwa faini kubwa jumatano hii na Mamlaka ya Maadili ya Sekta ya fedha ya Afrika Kusini kutokana na kosa la kuchapisha taarifa za uongo katika ripoti za fedha mwaka 2014 hadi 2016 na nusu mwaka 2017 na kuwapotosha wawekezaji wa kampuni ya Steinhoff, akilazimika kulipa randi milioni 475 (dola milioni 25.2, Tsh Bil 63).
Ripoti ya fedha ya Steinhoff ilifichua changamoto katika akaunti zake mnamo Desemba 2017, ishara ya kwanza ya udanganyifu kwenye ripoti uliosababisha anguko la kampuni hiyo. Steinhoff alipata hasara kubwa na mfululizo wa kesi tangu wakati huo.
Jooste aliambia uchunguzi wa bunge la Afrika Kusini mwaka 2018 kwamba hakufahamu kuhusu changamoto zozote za mahesabu alipoondoka kama CEO wa kampuni hiyo rmnamo Desemba 2017 Pia alikuwa chini ya uchunguzi kwa tuhuma za ufisadi na polisi wa Afrika Kusini.