Tajiri mkubwa nchini India bilionea Mukesh Ambani ameanzisha karamu za kifahari za kabla ya harusi ya mwanawe kwa kuwalisha zaidi ya watu 50,000 katika mji aliozaliwa, huku sherehe katika siku zijazo zikitarajiwa kujumuisha watu mashuhuri zaidi duniani.
Wakurugenzi wakuu wa teknolojia ya kimataifa, magwiji wa tasnia, mastaa wa Bollywood, wasanii wa muziki wa pop na wanasiasa wanatarajiwa kuungana siku ya Ijumaa kwa ajili ya sherehe kuu za siku tatu zinazoandaliwa na bilionea Mukesh Ambani, ambaye anajenga jumba kubwa la hekalu la Hindu kwa hafla hiyo.
Ambani, 66, mwenyekiti wa kampuni kubwa ya mafuta kwa mawasiliano ya Reliance Industries, ndiye mtu tajiri zaidi barani Asia kulingana na orodha ya mabilionea ya Forbes, yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 114.
Siku ya Jumatano jioni, Ambani na mkewe Nita pamoja na mwanae wAnant na mchumba wake Radhika Merchant walizindua karamu ya siku tatu kwa wanakijiji katika Mji wa Reliance katika mji aliozaliwa wa Jamnagar, katika jimbo la magharibi la India la Gujarat.
Ambani alifanya harusi ya bei ghali zaidi nchini India kwa binti yake mnamo 2018, ambayo inasemekana iligharimu dola milioni 100 huku mwanamuziki maarufu wa Marekani Beyonce akitumbuiza sherehe hiyo.