AyoTV imefanya mahojiano Chris Lukos ambaye ni mzaliwa wa Isanga Mkoani Mbeya, Umri wake ni miaka 51, elimu yake ni kidato cha nne baada ya kumaliza alijunga na Jeshi la Polisi ambapo alifanya kazi ya Polisi kwa miaka 5 tu akaacha na kwenda kuanza kuendesha malori Tanzania na baadae akahamia nchini Botswana na hatimaye Uingereza ambapo aliingia Uingereza akiwa na miaka 27.
“Ukienda Uingereza kama sio Proffesional mwanzo ni mgumu sana, nimeanza kwa kuosha vyoo, kusaidia mafundi, nimefanya kwenye Watehouse, baadae nikapata kazi Serikalini Westminster Council nikafanya kazi kwa miaka mitano nikarudi kwenye biashara” Lukos
Chris Lukos ni CEO wa Kampuni ya KC ameweka muda wake, akili yake, nguvu na pesa zake kwenye biashara ya uuzaji magri na bidhaa za majumbani alianza kampuni yake kwa kuwa na birika tano, microwave mbili, sufuria akajaribu mnada LIVE Facebook watu wakania na anakuambia vitu hivyo alipewa kwa mali kauli yaani alikopa.
Lukos sasa anamiliki Kampuni inayouza magari na bidhaa mbalimbali za majumbani kutoka nchini Uingereza na kuleta Tanzania kwa mwezi anaingiza kontena zaidi ya 20.
Yeye ni Muumini wa kufanya kazi anaamini kazi ndio kipimo cha Utu akimaanisha utu wako utathaminiwa ukifanya kazi amejiri Vijana 20
“Vijana tufanye kazi Mimi ni mgonjwa wa kisukari lakini muda wote nipo kazini mvua inyeshe hata jua liwake na simamia kazi yangu” Chris Lukos