Nakukutanisha na Rapha Group Limeted kutokea Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Mbeya ambae leo hii anaeleza namna anavyowakopesha Wakulima Wadogo Fedha kupitia Benki ya Kilimo.
‘Hii kazi isichukuliwe kama kazi ya Wazee hii kazi ni ya vijana ya watu wa lika la watu wote popote unaweza ukapata fedha, kwakweli soko sasahivi Dunia imefunguliwa na hasa Mama Rais wetu Samia Suluhu Hassan alipochukua nchi ameruhusu mataifa kuja na sasa hivi Masoko yapo wazi, Nchi nyingi zinataka mazazo kutokea hapa Tanzania’- Raphael Simon Ndelwa
‘Tukishirikiana na Benki ya Kilimo sasa hivi tumewakopesha Wakulima wanaozidi Elfu 2000 ambapa Pesa hivi zitaenda kuwasaidia na kukuza kile wanachokifanya na awamu nyingine tutaitangaza’- Raphael Simon Ndelwa
‘Tumefanya hivi ili Wakulima wadogo wadogo waweze kusambaza mbegu isambaze kwahiyo ni Fedha zinazotoka katika Benki ya Wakulima’- Raphael Simon Ndelwa
‘Zao la Mpunga linaumuhimu sana hapa nchini ukiacha la Mahindi na hapa watu wanakuja watu mbalimbali na sasa hivi kuna mashine ya kisasa ambayo inauwezo wa kuzalisha tani 45 kiukweli ni kitu kibwa sana’- Raphael Simon Ndelwa
KAMA ULIMISS MAHOJIANO ALIYOWAHI KUFANYIWA NA AYO TV UNAWEZA UKABONYEZA PLAY KUTAZAMA