Fahamu mambo sita muhimu kuhusiana na Bilioni 15.9 zilizotumika kwenye Umeme Mgodi wa Stamigold.
> Mradi ulikamilika Aprili 20, 2023 na STAMIGOLD kuanza rasmi kutumia umeme wa gridiyaTaifa Aprili 26, 2023.
> Njia ya umeme iliyojengwa ni ya ukubwa wa kilovoti 33.
> Njia ni ya umbali wa kilometa 105 kutoka kituo cha kupokea umeme cha Mpomvu – Geita.
> Ujenzi umehusisha njia ya kusafirisha umeme pamoja na kituo cha kupokea na kupoza umeme cha STAMIGOLD.
> Kituo kimejengwa kwa transfoma mbili zenye uwezo wa MVA 10 kila moja, na transfoma mbili za MVA 2.5
> Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo ACP. Advera Bulimba ametoa wito kwa wawekezaji kuwekeza Wilayani humo kutokana na uwepo umeme wa uhakika.