Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashimu Mgandilwa amesema kuwa serikali ya wilaya ya Tanga inajenga soko kubwa la kisasa kwaajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama wamachinga.
Dc mgandiliwa aliyasema hayo mara baada ya ziara yake ya kutembelea maendeleo ya ujenzi wa soko hilo linalo jengwa kwa fedha kutoka serikali kuu ili kuweka mazingira bora ya ufanyaji wa biashara kwa wafanyabiasha wadogo wadogo.
“Tunafahamu wafanyabiashara wadogo wadogo jijini Tanga wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya kukosa soko la Kisasa kwani kwa sasa wengi wao wanatumia Gulio la Tangamano ambalo sio salama sana kwao kutokana na eneo hilo kuto kuwa na miundombinu rafiki kwao kama vile vibanda vya kuhifadhi bidhaa zao na hivyo kuviweka chini hali ambayo sio salama “.Alisema Mgandilwa
Aidha alisema kuwa soko hilo litakaponkamilika litasaidia zaidi ya wafanyabiashara miatisa kufanya biashara zao sikuzote za juma nasio siku tatu kama ilivyo sasa kwenye eneo walilopo na kusisitiza kuwa hata kwaupande wa serikali ya jiji itakuwa na uwakika wakukusanya mapato kutokana na kodi zitakazo lipwa na wafanyabiashara hao.