Shilingi bilioni hamsini na mbili milioni mia tano arobaini na tano, miambili therasini na saba na senti hamsini na sita (52,545,237,056.00) zinakadiliwa kukusanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kwa mwaka wa fedha 2024/25 mapato ya ndani ikiwa ni shilingi bilioni sita milioni miatano sitini na tano, laki tano na tisini na nane (6,565,598,000.00) huku Ruzuku kutoka Serikali kuu ikiwa shilingi bilioni arobaini na tano milioni miatisa sabini na tisa, laki sita therasini na tis ana senti Hamsini na sita (45,979,639,056.00).
Hayo yamebainishwa katika kikao cha bajeti cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Morogoro cha kupia na kupitisha bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Akizungumzia bajeti hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri Joan Kataraia, amesema fedha hiyo imegawanyika katika maeneo mawili ambapo kwenye mapato ya ndani shilingi bilioni sita milioni miatano sitini na tano, laki tano na tisini na nane (6,565,598,000.00 itakuwa inachangia asilimia 60 kwa 40 ambapo 60 matumizi mengineyo na 40 itakuwa kwenye miradi ya maendeleo.
Katika mgawanyo wa fedha hizo kutakuwa kuna asilimia 10 ambayo itaenda kwenye vikundi vya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu na fedha nyingine itakuwa imepelekwa katika sekta ya Kilimo, Elimu, Afya pamoja na viwanda na biashara.
Ruzuku kutoka Serikali kuu zaidi ya bilioni arobaini na tano nukta tisa (45.9) mchanganuo ikiwa na mchanganuo wa malipo ya mshahara shilingi bilioni, zaidi ya bilioni therasini na moja nukta mbili (31.2), fedha za miradi, zaidi ya bilioni kumi na tatu nukta tatu (13.3) na matumizi mengineyo ni zaidi ya bilioni nukta nne (1.4).
Aidha Kataraia amesema “Tumejipanga kukusanya fedha hizi za mapato ya ndani kwasababu tumejiwekea mkakati kama Halmashauri wa kuwekeza zaidi kwenye kilimo kwasababu sisi tunategemea sana kilimo ambapo tumeweka fedha ya kutosha kwaajili ya kuiendeleza na kuboresha sekta ya kilimo lakini pia katika kilimo hapo tumepanga kutoa elimu kwa wakulima kufanya kilimo cha kisasa lakini pia kutumia zana sahihi katika kilimo na huku tumewekeza zaidi kwenye mazao ya viungo, kama karafuu, abdalasini, na viungo vingine pia tumejiwekeza ktika zao la michikichi ni zao la muda mrefu kidogo lakini tunaamini litakuwa na matokeo mazuri kwa hiyo tutawashawishi wakulima walime ili waweze kujitengenenzea kipato”.
Pamoja na bajeti hiyo kugusa sekta mbali mbali lakini pia Halmashauri inalenga kujenga kitega Uchumi katika Kata ya mvuha ambayo nayo itakuwa Sehemu ya ungizaji kipato pamoja na kutarajia kujenga machinjio ya kisasa ambapo kupitia sekta ya mifugo itasaidia kukusanya pesa na wananchi wataweza kuwa na uhakika wa kupata nyama safi.
Kataraia amesisitiza kuwa Halmashauri itaendelea kusimamia makusanyo yote kwa kuhakikisha kwamba mianya yote ya utoroshaji fedha itazibwa kikamilifu kwa bidhaa mbali mbali ili kusaidia kuwa na makusanyo mazuri yatakayopelekea hadi kufikia hiyo 2025 fedha hiyo itakuwa imekusanywa.
Msisitizo wa Mwenyekiti wa Halamashauri hiyo Lucas Lemomo kwa madiwani wake ni kusimama imara kila mtu kwenye kata yake ikiwemo kufanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi na kupokea taarifa zote muhimu zinazohitajika kwenye utekelezaji wa mradi husika.
Aidha Lemomo amesema…”Miradi ambayo imeanza utekelezaji wake 2023/24 na inahitajaika kukamilika mwezi wa sita mwaka huu ipewe kipaumbele na kila diwani ahakikishe anasimamia kikamilifu kwa kuwa na taarifa sahihi za miradi ilipo kwenye kata yake na kujua kwanini imechelewa kukamilika na kama kutakuwa taarifa za uzembe wowote au rushwa basi taarifa zitolewe kwa mkurugenzi wa Halmashauri au mwenyekiti kwa hatau zaidi zicweze kuchukuliwa”.
Melekezo ya Chama cha Mapinduzi CCM ngazi ya Wilaya ambayo yametolewa na Gerold Mlenge, Mwenyekiti CCM Wilaya ya Morogoro ni Halmashauri kuja na mipango mikakati mipya ya kuvutia wawekezaji hasa kwenye sekta ya kilimo na Viwanda biashara ili kuiwezesha halmashauri kuwa na vyanzo vya uhakika na vya kudumu vya mapato.