Bilionea na mwanzilishi wa Kampuni ya Microsoft, Bill Gates amesema kuwa dawa ya virusi vya corona itakapopatikana inapaswa kusambazwa kwa wahitaji na sio kwa watu wanaoweza kuinunua kwa bei ya juu zaidi.
Gates ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye mkutano unaohusu virusi vya corona ulioandaliwa na Jamii ya Kimataifa ya kushughulikia Virusi vya Ukimwi , wikendi iliyopita.
“Kama dawa hizo zitapatikana na kusambazwa kwa wenye uwezo wa kuzinunua kwa bei ya juu badal aya watu na maeneo yenye uhitaji zaidi, tutakuwa na janga lingine kubwa na la muda mrefu na litasababisha vifo zaidi,” Bill Gates.
“Tunahitaji viongozi wetu wafanye maamuzi magumu kuhusu kusambaza kwa usawa, sio kwa kuzingatia nguvu ya soko,” Gate
Kauli ya bilionea huyo Mmarekani imekuja kufuatia uamuzi wa Serikali ya Marekani kununua karibu kiasi chote cha dawa ya remdesivir, ambayo imethibitika kuwa na ufanisi zaidi katika kuwasaidia wagonjwa wa corona kupona haraka.
Wakati huo, nchi nyingi zenye nguvu zaidi za kiuchumi zimewekeza mabilioni ya dola za Marekani katika utafiti wa dawa ya corona, hali inayoibua maswali kama watakubali kuigawa kwa nchi nyingine kwa usawa baada ya kuibaini.
Gates alisisitiza kuwa dunia itaweza kupambana na corona kama itaungana pamoja, kama ilivyokuwa kwa mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi.