Bodi ya mikopo ya elimu ya juu Tanzania (HESLB) imesema serikali imetenga zaidi ya bilioni 700 kwa mwaka huu wa 2024,2025 kwaajili ya kusomesha wanafunzi zaidi ya 240,0000 kwa wanafunzi mbalimbali wa vyuo vikuu
Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya mikopo Dkt.Bill Kiwia amesema serikali imeendelea kuboresha bajeti ya kusomesha wanafunzi na wanatarajia pia kuongeza idadi ya wanufaika wa mikopo kwa asilima 20 na sasaivi kupitia bodi ya mikopo wanasomesha wanafunzi zaidi ya 240,0000 ambapo ni sawa na asilimia 70 ya wanafunzi wote na mwakani watasomesha wanafunzi zaidi ya 245,0000
“ kwanza nimshukuru Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza kwenye elimu na ni jambo kubwa na serikali imeendelea kusomesha na mwaka huu tutaendelea kuongeza idadi ya wanufaika wa mikopo kwa asilimia 20” Amesema Bill kiwia
Hatahivyo Dkt.Bill Kiwia amesema kasi ya ukusanyaji wa mikopo imeongezeka na kwa mwezi wa 7 tiari wameshakusanya zaidi ya bilioni 17 na akisisitiza urudishwaji wa mikopo kwa watu ambapo bado hawajarejesha mikopo
siku ya leo mkurugenzi mtendaji wa bodi ya mikopo Tanzania Dkt Bill Kiwia ametembelea vyuo vyote vinavyopatikana mkoani iringa lengo ni kuzidi kuimarisha mahusiano baina ya bodi pamoja na vyuo