Jackline Shirima ni msichana ambaye ana umri wa miaka 21 lakini anadai aliugua ugonjwa wa ‘gangrene’ ambao ulisababisha kukatwa miguu yote miwili kwa wakati mmoja ambapo baadaye alijitokeza nakuomba msaada ili aweze kupata miguu ya bandia nakuweza kutembea tena kama awali.
“mchango niliokusanya ni million tatu na laki nane, kwa hiyo sasa hivi imebaki million tatu na laki tano ili tuweze kufanikisha niweze kupata miguu,amejitokeza msamaria mwema baada ya ile video akanilipia chupa kwa mwezi mmoja karibu na hospitali,miguu imeshafika nchini wiki ijayo kama hela itakuwa imekamilika nitapata miguu”-Jack