Binti wa mwisho wa hayati Nelson Mandela, Zindzi Mandela aliyefariki dunia nchini Afrika Kusini mapema wiki hii alikuwa na maambukizi ya virusi vya corona, Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini SAB imeripoti taarifa hiyo.
Mtoto wa Zindzi, Zondwa Mandela amethibitisha kuwa ni kweli mama yake alikutwa na COVID19, amesema hawajui alipopata ugonjwa huo na familia yake inasubiri ripoti ya uchunguzi.
Zindzi ambaye ni mtoto wa 6 wa Mandela alikuwa Balozi wa Afrika Kusini nchini Denmark, anatarajiwa kuzikwa baadae leo.