Wanawake nchini Poland wameandamana kupinga serikali ya nchini hiyo kupitisha sheria mpya ambayo itakataza moja kwa moja utoaji mimba wa aina yoyote ile.
Wanawake hao wakiwa wanaandamana pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu wameeleza kuwa kutoa mimba kukifanywa haramu kutahatarisha maisha ya wanawake ambao maisha yao yanakuwa hatarini kutokana na kubeba ujauzito.
Takribani mashirika yasiyo ya kiserikali 200 yamejiunga kwenye harakati hizo za kupinga serikali kukataza utoaji wa mimba, kwa kuandika waraka wa rufaa kwa Bunge la nchi hiyo likisema sheria hiyo itahatarisha maishaya wanawake.
Waraka huu pia umeungwa mkono na Ofisi ya Tume Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.
ON AIR: Mshahara wa kwanza wa Waziri January Makamba mwaka 94