Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Anthony Blinkenamesema alizungumza na Rais wa Niger Bazoum ambaye kwa sasa nanashikiliwa na kumueleza ‘’juhudi zetu zinazoendelea za kupata suluhu la amani kwa mgogoro wa sasa wa kikatiba.
Katika ujumbe wake wa Twitter Bw Blinken aliandikakuwa ‘’Marekani inasisitiza wito wetu wa kuachiliwa mara moja kwake na familia yake’’.
Awali Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani alisema kuwa hafikirii Urusi au Wagner ndiyo zilizochochea mapinduzi ya Niger.
Hata hivyo Marekani ilikuwa na wasiwasi kuhusu kundi hilo “labda kujidhihirisha” katika sehemu za ukanda wa Sahel, alikiambia kipindi cha BBC Focus on Africa.
Ecowas, jumuiya ya kiuchumi ya mataifa 15 ya Afrika Magharibi ilitoa makataa ya Jumapili kwa viongozi wa serikali ya Niger kujiuzulu na kumrejesha Rais Bazoum.
Tarehe hii ya mwisho ilipuuzwa na Ecowas inatazamiwa kufanya mkutano siku ya Alhamisi ili kuamua nini cha kufanya baadaye.
Siku ya Jumatatu, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Victoria Nuland, alifanya kile alichokitaja kuwa “mazungumzo magumu na ya wazi” na viongozi wa mapinduzi, ambao alisema wanaelewa hatari ya kufanya kazi na mamluki.
Bw Bazoum, ambaye kwa sasa yuko kifungoni, pia amezungumzia wasiwasi wake kuhusu ushawishi wa Wagner barani Afrika.