Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken siku ya Alhamisi alizitaka Israel na Hamas kukamilisha makubaliano ya usitishaji vita Gaza, akisema kwamba “asilimia 90” ya makubaliano “yamekubaliwa”.
Blinken aliongeza kuwa Marekani itatoa mawazo zaidi kupitia Misri na Qatar. Hata hivyo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alikanusha madai hayo katika mahojiano na Fox News, akisema “sio karibu”.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken siku ya Alhamisi alizitaka Israel na Hamas kukamilisha makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza, akisimama na tathmini ya Marekani kwamba asilimia 90 ya makubaliano yalikuwa tayari.
Blinken alisema kuwa Marekani itatoa mawazo zaidi katika siku zijazo kupitia wapatanishi Misri na Qatar kwa matumaini ya kusaini makubaliano.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika mahojiano na Fox News siku ya Alhamisi alikanusha tathmini ya afisa wa Marekani kwamba asilimia 90 ya makubaliano yalikuwa tayari, akisema “sio karibu.”
Lakini Blinken alirudia tathmini hiyo katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa ziara yake nchini Haiti, akisema, “Nadhani kulingana na kile nimeona, asilimia 90 imekubaliwa.”