Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alionya siku ya Jumatatu kwamba msukumo wa hivi punde zaidi wa kusitishwa kwa mapigano Gaza na mpango wa kuachiliwa kwa mateka pengine ni fursa bora na ikiwezekana ya mwisho, akizitaka Israel na Hamas kufikia makubaliano ambayo hayana ukomo.
Kundi la Waislam wa Palestina Hamas limetilia shaka uwezekano wa kufikia makubaliano tangu mazungumzo ya Qatar wiki jana yalipositishwa bila mafanikio, lakini mazungumzo hayo yatarejea wiki hii kwa kuzingatia pendekezo la Marekani la kuafikiana.
Blinken alikutana na Rais wa Israel Isaac Herzog siku ya Jumatatu kabla ya kuelekea kwenye mkutano na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wakati huko Gaza majeshi ya Israel yalitinga zaidi katika Khan Younis, wakaazi walisema, katika awamu ya hivi punde ya shambulio lao.
“Huu ni wakati wa maamuzi, pengine bora zaidi, labda fursa ya mwisho ya kuwarudisha mateka nyumbani, kupata usitishaji mapigano na kuweka kila mtu kwenye njia bora ya kudumu kwa amani na usalama,” Blinken aliwaambia waandishi wa habari kabla ya kukutana na Herzog.