Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Augustino Mahiga leo July 24, 2017 amekutana na Waandishi wa Habari na kusema Tanzania haijawahi kujihusisha na masuala ya uchaguzi wa Kenya na haina mpango wa kufanya hivyo.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa kadhaa ambazo zimekuwa zinadai kuwa Tanzania inaingilia masuala ya Uchaguzi wa Kenya ambao utafanyika mapema mwezi ujao.
“Kwa taarifa nzuri tulizotoa za uhusiano wetu leo na mimi na Waziri mwenzangu kukutana katika hali ya urafiki na kabla ya hapo Marais wetu kuzungumza kwa undugu na kwa urafiki na ujirani mwema hakuna mtu ambaye anatakiwa awe na wasiwasi kuhusu mahusiano yetu mazuri kati ya Viongozi wetu, Serikali zetu na watu wetu wa mataifa haya mawili.
“Ni siasa ya Tanzania kutokuingia ndani siasa za nchi nyingine. Ni siasa ya Tanzania kuwa na marafiki wote sio tu wa kiserikali lakini pia marafiki na kutambua vyama mbalimbali kisiasa. Sisi Tanzania hatujawahi, hatukuthubutu na hatutathubutu kuingilia siasa za nchi nyingine na hasa nchi jirani marafiki kama Kenya.
“Nataka hii ifahamike kabisa na tunasema kwa uhakika kabisa ni Serikali ambayo daima imekuwa karibu na Serikali ya Kenya. Suala la uchaguzi na kuhesabu kura ni suala la Wakenya. Hatujawahi kuingiliana, Kenya haijawahi kuingilia Tanzania, Tanzania haijawahi kuingilia Kenya. Kwa nini leo iwe hivyo? Sisi tuna utaratibu wetu wa Afrika Mashariki tunatembeleana tunafanya kazi pamoja kwa nini iwe hivyo?” – Balozi Augustino Mahiga.
Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Mahiga amesema Tanzania haijawahi kujihusisha na masuala ya uchaguzi ya Kenya na haina mpango wa kufanya hivyo pic.twitter.com/hV4sFfEgCr
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
“Wabunge hatufanyi tuliyowaahidi Wananchi” – Dr. Tulia.
Kitu Zitto Kabwe ameongea mbele ya Rais Magufuli Kigoma…play kwenye hii viedo hapa chini kutazama!!!